Polisi wa Kenya wanasema kuwa wanaendelea na uchunguzi, juu ya mauaji
ya balozi mpya wa Venezuela nchini humo, ambaye aliuwawa Ijumaa. Olga
Fonseca, aliyeanza kazi Kenya kati ya mwezi Julai, alikutiakana
ameuwawa nyumbani kwake, na watu sita wamekamatwa hadi sasa.
Watu hao sita wamekamatwa siku mbili tu baada ya balozi huyo kupatikana amefariki nyumbani kwake.
Siku ya Ijumaa, polisi walisema kuwa maiti ya Bi Olga Fonseca
ilipatikana kitandani mwake lakini sababu za kuuwawa kwake hadi sasa
hazijulikani.
Bila ya kutoa maelezo zaidi, polisi wamesema kuwa wanawashikilia watu sita kuhusiana na kifo cha balozi huyo.
Taarifa kutoka wizara ya maswala ya njee ya Kenya imesema kuwa
wafanyikazi katika makaazi ya balozi huyo waliwasilisha malalamiko yao
kwa polisi baada ya kufutwa kazi hivi majuzi.
Inadaiwa kuwa bi Fonseca aliwafuta kazi baada ya wao kukataa kuondoa
malalamiko kuhusu madai ya kunyanyaswa kijinisia na mtangulizi wa balozi
huo.
Hata hivyo polisi wamesema wanachunguza madai hyao.
BBC Swahili |
No comments:
Post a Comment