Askofu Edinburg Mdegela, askofu mkuu wa dayosisi ya Iringa |
Siku
yoyote kuanzia Jumatatu ya Julai 23, Askofu wa KKKT Dayosisi ya
Iringa, Dk Mdegella ataitwa Mahakamani kujibu madai ya kumfukuza bila
kufuata utaratibu Mchungaji Lambert Mtatifikolo wa dayosis hiyo.
Taarifa kutoka kwa wakili wa mchungaji huyo, Wakili Alfred Kingwe
zitakazokujia kwa kina , zimedai kwamba Askofu Dk Mdegella alianza
kutafutwa wiki iliyomaliza leo na maafisa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
ya Mkoa wa Iringa ili akabidhiwe hati ya kuitwa mahakamani. Hata hivyo
Askofu Dk Mdegella hakupatikana, lakini taarifa za uhakika kutoka kwa
wakili huyo zimedai kwamba atapewa hati hiyo siku yoyote wiki
inayoanza leo. chanzo:http://www.frankleonard.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment