FOLLOWERS

Sunday, June 3, 2012

TAKUKURU YAMFIKISHA IDD SIMBA KIZIMBANI

Waziri wa zamani wa viwanda na biashara Mzee Idd Simba, kulia akiwa na wakili wake mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam alipopelekwa kusomewa mashtaka yake                              ( picha kwa hisani ya Raia Mwema)
Mzee Idd Simba ambaye amepata kuwahi kuwa waziri wa viwanda na biashara, jumanne ya tarehe 29 alifikishwa katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaa akikabiliwa na mashtaka mbali mbali ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara.Kushitakiwa kwa Idd Simba kunatokana na kashfa iliyopata kurindika kuhusu UDA, kashfa ambayo baada ya kuibua mjadala mkali bungeni, ilifanyiwa uchunguzi na Kampuni ya KPMG. Hata hivyo Idd Simba alipata dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana hiyo.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...