FOLLOWERS

Saturday, June 9, 2012

OKWI NA NIYONZIMA KUKWAANA KATIKA TUZO

Mshambulia wa Simba Emmanuel Okwi akishangilia moja ya magoli aliyoifungia timu hiyo

Haruna Niyonzima alipokuwa akitambulishwa rasmi katika timu hiyo ya jangwani

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Uganda na timu ya Simba, Emmanuel Okwi, watachuana na kiungo wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda na Yanga Haruna Niyonzima kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka kwa wachezaji wa kigeni nchini inayosimamiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).
Mwingine wa kigeni alioingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni na Kipre Tchetche wa Ivory Coast anayechezea Azam FC.
Akizungumza katika hafla fupi ya kutaja majina ya wachezaji wa ndani na nje watakaowania tuzo hizo, Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo Masoud Sanan alisema kwa upande wa wanasoka wazalendo, wanaowania ni John Bocco, Aggrey Morris wote wa Azam na Juma Kaseja wa Simba.
Kwa kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje ya nchi ni Henry Joseph wa Kongsvinger ya Norway na Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...