Kama
kuna ,makosa ambayo watanzania tunafanya basi ni pamoja kumchagua mtu kuwa
mbunge eti tu kwa sababu alitoa milioni mbili mfukoni mwake na kuchangia
uchimbaji wa kisima au ujenzi wa darasa. Kuchangia shughuli za maendeleo katika
maeneo yetu sio jukumu la mbunge, mbunge ana kazi kuu nne zifuatazo;
- Kuunganisha watu wake na serikali
- Kukusanya shida za watu wake na kurudisha majibu
- Kufikiria sheria mpya
- Kuisahihisha serikali ili itie juhudi zake zote kutimiza hoja za watu.
Wajibu wa mbunge
- Kuangalia na kutambua shida zinazowakabili wananchi wake.
- Kuwaheshimu wananchi wake.
- Kushirikiana na wananchi wake katika kazi mbali mbali za kujenga taifa
- Kushirikiana na viongozi wa sehemu yake, wilaya na mkoa wake.
- Kuisaidia serikali itawale vizuri.
- Kuhudhuria mikutano ya bunge.
No comments:
Post a Comment