FOLLOWERS

Tuesday, July 31, 2012

MBUNGE WA ZAMANI WA BUSEGA AVAMIWA

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega wilayani Magu, Dk. Raphael Chegeni,

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega, Wilayani Magu, Jijini Mwanza, Dkt. Raphael Chegeni, 'amelizwa' vitu vyake kadhaa ikiwamo na bastola yake.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi, kinasema kuwa Dkt. Chegeni ameibiwa usiku wa kuamkia leo, baada ya watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, kuvunja Ofisi ya mheshimiwa huyo.

Aidha imelezwa kuwa Majambazi hayo baada ya kuvunja mbali na kuchukua Baastola hiyo, pia wameondoka na Kasha maalum la kuhifadhia Fedha pamoja na Laptop iliyokuwa mezani.

Ikithibitisha tukio hilo, polisi mkoani Mwanza, imesema wezi wamekomba sh. Milioni 5 za madafu na Dola 13 za Kimarekani zilizokuwa kwenye sefu hiyo.( KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO)

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...