Ndege ya kijeshi ya Uturuki |
Serikali ya Uturuki inafikiri
kuwa ndege yake moja ya kijeshi iliyogunguliwa na Syria Ijumaa, pengine
iliingia katika anga ya Syria.Rais Abdullah Gul, aliliambia shirika la habari
la Uturuki, Anatolia, kwamba ni kawaida kwa ndege za kijeshi kuvuka mipaka ya
nchi, zinaposafiri kwa kasi.
Bwana Gul alisema serikali yake inawasiliana
na Syria kuhusu tukio hilo.Majeshi
ya wanamaji ya nchi zote mbili yanafanya msako wa pamoja kuwatafuta marubani wa
ndege hiyo.Uturuki ilimundosha balozi wake nchini Syria
mwezi wa March baada ya ghasia kuzidi nchini humo, lakini Bwana Gul alisema
hiyo haizuwii serikali yake kuwasiliana na serikali ya mjini Damascus.
No comments:
Post a Comment