FOLLOWERS

Saturday, June 2, 2012

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA BAHATI NZEMA

Bahati Nzema ambaye mnamo tarehe 20 mwezi wa kwanza alimpoteza baba yake mzazi mzee Victor Nzema. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi..amen

Salamu zangu za rambi rambi kwako..BH

HISIA ZANGU.
1. Naandika utenzi huu
Kwako BH rafiki yangu
Zinenapo hisia
Midomo huwa bubu
Ni pigo limekufika
Yapasa umuombee thawabu

2. Atakuwa aso akili
Binadamu dhahili
Baba ni muhimili
Leo hayupo fikiri
Angependa kunena nawe
Katu kauli siyo yake

3. Ni habari za kusikitisha
Baba katutoka ghafla
Afadhali ya msiba
Uwe wa mwenzio
Chungu ya msiba
ukufike wa kwako

4. Pole zangu ni nyingi
kukupa wangu rafiki
haitoshi moja siku
itanichukua nyingi siku
zinenapo hisia
midomo huwa bubu

5. Kifo ni fumbo fikiri
Huja usipofikiri
Tena una matumaini
Katika yako safari
Hata kwangu kumbukumbu
2011, 31 januari

6. Kwa hili naandika
Nashindwa kutamka
Nauhisi wako uchungu
Rafiki uliokushika
Unapomlilia baba
Kumbuka kuna kesho

7. Wewe yakungoja
Si yake tena baba
Si hiyana uchungu lazima
Hili lapita tambua
Lijalo hujalitambua
Kesho yaja BH
Simama kiume rafiki

8. Nafasi ya wazi
Kuiziba ni kazi
Yakubidi ufanye kazi
Kuuziba huo uwazi
Ni ngumu kufanikiwa
Ukifanya utaweza

9. Rehema za mungu
Ziko nasi wahitaji
Kabla ya kunena
Jalali aliyajua tutakayo
Zinenapo hisia BH
Midomo huwa bubu

10. Sio tu kiume
Bali yakubidi usimame
Taa moja izimikapo
Nyingine huwashwa papo
Tazama utokako
Kuwa makini uendako

11.Utokako ulishikwa
Uendako jishike
Simama na imani
Furaha atapata baba
Hatoweza tu kwambia

12.Tambua kibinadamu
Adui mkubwa kifo
Yatuusia maandiko
Kubatilishwa atakuw wa mwisho
Ni nini utakiona BH
Ni kufutwa kwa uchungu

13. Utashi wa kibinadamu
Mbali haudumu katu
Angelijua baba yetu
Asingeenda safari katu
Sauti yake ikiita
Rafiki wote twaitika
Nangoja yangu nami itafika

14. Naandika haya hisiani
Kukupa pole rafiki
Ni kwa kumbukumbu
Ya baba VICTOR NZEMA
Namuombea yaliyo mema
Katika ujao huo uzima

15. Hisia rafiki yangu
Ni chungu moyoni mwangu
Nagota mkono wangu
Kwako hizo pole zangu
Baba katangulia rafiki yangu
Tumuombee rehema kwa mungu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...