Rais wa mpito wa Mali Dioncunda Traore |
Mali inaelekea kutereza kuingia
kwenye ‘mgogoro wa haki za binadamu’ Shirika la Kimataifa la Amnesty
International limeonya.
Jeshi limekuwa likijihusisha na maamuzi ya
mauaji, mateso, na udhalilishaji wa kijinsia tangu mapinduzi ya mwezi Machi,
linasema, na kutaka uchunguzi ufanyike.
Jeshi limetoa mamlaka kwa serikali ya mpito
lakinibado lina ushawishi mkubwa.
Mali ligawanyika kwenye makundi mawili baada
ya mapinduzi huku Kaskazini ikidhibitiwa na wapiganaji wa Kiislam na waasi wa
Tuareg.
Wakati huo huo Shirika la Msalaba Mwekundu
(ICRC) limezungumza na maafisa wa jeshi 79 wanaoshikiliwa na Vuguvugu la waasi
wa Uhuru wa Azawad (MNLA), lilisema.
Ziara hiyo ililenga kuwapatia nafasi
wafungwa baada ya miezi ya kukaa kifungoni, mkuu wa ICRC Mali Jean-Nicolas
Marti amenukuliwa na shirika la AP likisema.
‘Hatua lazima zichukuliwe kuhakikisha kuwa
waliofanya mapinduzi ‘hawaendelei na ukatili wao,’Amnesty International
lilisema.
"Tuko wanne. Walitutaka tutoe nguo zetu
zote. Tuliambiwa tungiliane kimwili sisi kwa sisi, la sivyo wangetuua
wote," Afisa mmoja amenukuliwa akisema na shirika la Amnesty.
Takriban askari 21 hawajulikani waliko tangu
kwa kujaribu kupinga mapinduzi hayo mwezi April, Amnesty lilisema.
Limeongeza kuwa wafungwa wanalazimishwa
kukiri makosa baada ya kuteswa mikono yao ikiwa imefungwa nguo zao
zimesokomezwa midomoni na sigara zikizimwa masikioni mwao.
"Vitendo hivi vya kikatili vinapita
sheria za Haki za Biandamu Mali na hatua lazima zichukuliwe ili wanaofanya
ivtendo hivi wasiendelee’Amnesty lilisema.
Jeshi lilifanya mapinduzi baada ya serikali
ya kuituhumu kushindwa kumaliza uasi kaskazini.
Lakini waasi wa Tuareg na wapiganaji wa
Kiislam walitumia fursa hiyo ya mapinduzi na kushika maeneo makubwa ya
kaskazini.
Wapiganaji wa Kiislam wameharibu hifadhi za
kale za mji wa Timbuktu na kudharau maonyo ya Umoja wa Mataifa na makudni
mengine kuwa walikuwa wakifanya uhalifu.
No comments:
Post a Comment