FOLLOWERS

Wednesday, August 22, 2012

WATOTO WAMCHINJA BABA YAO KWA MAPANGA

watoto wengine wa marehemu, Nicko Mkini (kushoto) na Jofrey Mkini (kulia) ambao ndugu zao walimuua baba yao mzazi kwa kumkata na mapanga

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita akizungumza na
waombelezaji nje ya nyumba ya marehemu

hapa akitoa rambirambi kwa mke wa marehemu
WATU wawili, Nelson Mkini (37) na Cuthbert Mhegama Mkini (28), wamemuua kwa kumchinja kwa panga baba yao mzazi Ejid Mkini (65), kwa tuhuma kwamba amemloga mama yao mzazi anayeendelea kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na kuvimba miguu.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea majira ya saa 3.40 usiku nyumbani kwa marehemu huyo, katika kijiji cha Pomerini (Ng'uruhe), wilayani Kilolo, mkoani Iringa.


Baada ya tukio hilo, vijana hao walitokomea kusikojulikana, hata hivyo jeshi la Polisi limeanzisha msako mkali kuwasaka.


Wakati Nelson ni mkazi wa kijiji hicho, Cuthbert ni mwanafuni wa Chuo cha Ualimu Agafilo, kilichopo wilayani Njombe, mkoani Njombe.


Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita alitembelea kijijini hapo na kutoa msimamo wa serikali kuhusiana na mambo ya kishirikina kabla hajatoa pole kwa familia ya marehemu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...