Tanzania Journalists’ Association
(TAJA)
Malanga St. - Kinondoni, Duka la Habari House No. 102, Opposite Oil Com Station
THE PRESIDENT,
P.O.BOX
7447,
Dar
es Salaam.
Tel/Fax 255-222 760737
Mob:+255-764450000/719-222448
+255-786450000.
Email: tajahabari66@gmail.com
KWA WAHARIRI
WA
2 Augosti 2012
VYOMBO VYA HABARI
MAKINI
YAH:
TAMKO LA KITAALUMA KWA UMMA KUHUSU SERIKALI KULIFUNGIA GAZETI LA MWANAHALISI KWA MUDA
USIOJULIKANA:
NB: Kuandika habari bila
ATTRIBUTION(kumtaja source WAKO) na kushindwa ku-BALANCE Habari yako kwa MTUHUMIWA katika HABARI
unayoandika ni
ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu –MCQUAIL (2005).
Kwa sababu hiyo ya
MAADILI ya fani yetu,TAJA inalaani kwa nguvu zake zote gazeti la
MWANAHALISI na SERIKALI kwa kuwa VIRANJA
wa KUBINYA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI kwani hawa wawili ( MWANAHALISI NA
SERIKALI) ni MAADUI HATARI wa maendeleo
ya TASNIA YA HABARI na HADHI YA
Waandishi wa Habari wasomi na makini hapa
Nchini.
Aidha tunashangazwa sana na wale wote wanaoilaumu serikali kwa madai ya kwamba
inakandamiza uhuru wa habari na kutetea Gazeti la mwanahalisi eti wanadai linatumia
uhuru wa habari kama unavyoelezwa katika
katiba. TAJA tunaelewa watu hao wote wakiwemo wanaodaiwa kuwa NGULI wa tasnia
ya habari ni watu ambao elimu yao
ya TAALIMU YA HABARI INA MASHAKA au ni ndogo kiasi kwamba hawaelewi maana ya
uhuru wa vyombo vya habari kitaaluma duniani kote MAANA YAKE.
Duniani kote wasomi
wa tasnia ya habari wanajua vigezo vya kuwepo uhuru wa habari misingi yake
mikuu (1) Uandishi wa habari kwa kuzingatia misingi ya fani ya uandishi wa
habari (Journalistic genre ethics) ambapo habari yoyote ni lazima iwe na
ATTRIBUTION na pili BALANCE isipokuwa inaruhusiwa kuandika bila kutaja jina
kama kwa kufanya hivyo utahatarisha usalama wa mtoa habari (source). MWANAHALISI
ni MAHIRI katika kuandika habari za upande mmoja (UNBALANCED STORIES) na zinazohusu
tukio moja tu. MWANAHALISI kwa
kutozingatia maadili ya uandishi wa habari ni mvunjifu mkubwa wa uhuru wa
habari hapa nchini na anadhalilisha fani ya UANDISHI WA
HABARI NA WANAHABARI WENGINE MAHIRI (WATCHDOGS). TAJA Tuna wasiwasi na wale
wote wanaounga mkono uandishi wa habari za MWANAHALISI zisizo attribution NA Balance. MWANAHALISI
ukiwapa ushauri wa kitaaluma wepesi kuitikia lakini HAWATEKELEZI- Rais wa TAJA amewahi kuzungumza na Mhariri, ameishia
kuitikia kimaelewano lakini hakuna hatua aliyoichukua “kitaaluma” katika
ku-BALANCE habari za upande mmoja
wanazolalamikiwa.,
Hivyo TAJA hatutafuni
maneno na wala hatuoni haya kwamba wao ni WADHALILISHAJI WAKUBWA wa waandishi wa habari makini hapa Nchini na
ni WAVUNJAJI WAKUBWA WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI HAPA TANZANIA.Wanaowatetea
yawezekana wana AGENDA zao nyingine sio
ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari.
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI si ufunguo wa kuandika
habari zisizozingatia maadili na weledi wa uandishi wa habari. TAJA inawaomba
wale wote wanaotoa mchango kuhusu jambo hili wajiridhishe kwanza na kuijua fani
hii wasivyamie tu kama wanavyofanya ndugu zetu wa fani ya sheria eti wapeleke kesi mahakamani(mbona
waao mawakili wakivunja maadili ya uwakili hawawapeleki Mahakamani ila
wanawafukuza?),sisi tunawauliza kesi gani wakati MWANAHALISI habari zake
hazizingatii maadili GAZETI hili pia ni mkosaji kama serikali yenye sheria
KANDAMIZI. Hawa wawili hawana tofauti
wanalaumiana kwa makosa ambayo wote wanayafanya-wakandamizaji wa uhuru
wa habari Tanzania
kila mmoja kwa aina yake-hakuna wa KUTETEWA katika MGOGORO HUU.
SERIKALI nayo
TUNAILAANI kwa nguvu zetu zote, kwani
yenyewe inaongoza kwa ubinyaji UHURU WA HABARI hapa Nchini, ingawa washabiki wa
MWANAHALISI wanalalamikia sheria moja tu ya MAGAZETI YA MWAKA 1976 NO 3. Ukweli
ni kwamba hiyo inaoonyesha ufinyu wao katika kuelewa ukandamizaji wa Serikali
kwa Uhuru wa Habari. HAPA NCHINI.
SERIKALI YA TANZANIA
ni kandamizi sana ina zaidi ya sheria 20
ZINAZOBINYA UHURU WA HABARI NCHIN I, aidha hata ukiifuta hiyo sheria ya
mwaka 1976 ukaacha mlolongo nilioutaja
bado hujatatua tatizo la ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari Nchini. UTATUZI
ni kuandikwa sheria mpya ya upatikanaji habari na kufuta zote kandamizi zilizopo,lakini
SIO KUTETEA UANDISHI HOLELA WA AINA YA MWANAHALISI USIOZINGATIA JOURNALISTIC
GENRE ETHICS.
TAJA tunasema
wasiokuwa wasomi katika fani hii wasidandie HOJA HII NYETI yahitaji wasomi wa
fani hii ambao kwa sasa tupo na tumemaliza Vyuo vikuu sio mazoea eti mtu akiwa
mwandishi wa miaka mingi NGULI –mawazo hayo yamepitwa na wakati-TUSOME TUELEWE
VYEMA MAANA YA UHURU WA HABARI ILI TUELEWEKE DUNIANI SIO KUTETEA WAVUNJA
MAADILI YA FANI YETU-“TUNAJIAIBISHA WENYEWE MBELE YA WENYE WELEDI KAMA VILE
JIRANI ZETU KENYA”
TAJA TUNAWAOMBA
SERIKALI AMBAO NI WAONGOZAJI KATIKA
UBINYAJI WA UHURU WA HABARI WAFANYE HIMA KUPITISHA SHERIA YA UHURU WA HABARI NA
SHERIA HIYO LAZIMA IWE NA KIPENGELE CHA KUFUNGIA CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI
KISICHOZINGATIA MAADILI YA UA NDISHI WA HABARI
Tunazungumza kisomi
na tunaomba tueleweke,TAJA haiungi mkono sheria ya magazeti ya mwaka
1976,lakini kitendo cha kufungia gazeti lolote lisilozingatia maadili ya
uandishi wa habari hata baada ya kupewa
ushauri TAJA TUNAKIUNGA MKONO ili kuweka
heshima ya fani yetu,isiendelee kuchezewa kama kichwa cha MWENDAWAZIMU.
1). Tunaomba serikali
IUNDE jopo la wasomi wa fani ya habari kutoka CHUO Kikuu HURIA, UDSM, SAUT na TUMAINI
Iringa tukae na hao wanaotetea MWANAHALISI NA kulaumu SERIKALI peke yake ili
UMMA ueleweshwe jambo hili linavyopotoshwa na wanaojiita NGULI wa habari,
matatizo ya tasnia ya Habari Nchini imevamiwa na watu wasio Wataalamu wa Fani
hii na wengine hawana hata Diploma tu za fani ya Uandishi wa habari au
Mawasiliano ya UMMA lakini wamejipa majina ya NGULI (expert- kawaida mtu expert
anategemewa kuwa angalau na M.A kama si PhD na kadhalika kwani tulio nao hawana
hata Diploma zinazotambulika katika fani),ndio wanatupa taabu katika
kuharibuTasnia hii Nchini kwa kujifanya kwamba wanafahamu sana UHURU WA VYOMBO
VYA HABARI,KUMBE WANACHOFAHAMU NI KINYUME.
2) Tunaomba wale wote
wanaojitokeza na kujitambulisha kuifahamu fani ya habari na dhana ya uhuru wa
habari wasiwe wanazungumza kiholela hii ni fani yenye wasomi, hivyo pia
watutajie C.V zao ili tujiridhishe na maoni yao tujue ya kitaalamu au ya aina ya kijiweni?
“MWANAHABARI MSOMI
HAWEZI HATA KIDOGO KUTETEA “UNETHICAL WRITTEN NEWS PAPER”
TAJA TUNARUDIA KULAANI WOTE, MWANAHALISI NA SERIKALI KWA MATENDO YAO
YA UKANDAMIZAJI MKUBWA WA UHURU WA KUPATA HABARI NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.
NI MATEGEMEO YA TAJA KWAMBA,MAADUI HAWA
WAWILI WALIOJITAMB ULISHA WAZI WAZI WATAJIREKEBISHA KWA SERIKALI KUPELEKA SHERIA
YA UHURU WA VYOMBO YA HABARI BUNGENI NA KUANCHANA NA AHADI ZISIZOTEKELEZEKA(HEWA)
KILA MWAKA NA MWANAHALISI NAO WAJIENDELEZE KITAALUMA ILI WAJUE DUNIANI HAKUNA
POPOTE KWENYE UHURU WA HABARI USIO MIPAKA.
MWISHO. TAJA tunampongeza Mhe. Saed Kubenea Mkurugenzi wa
MWANAHALISI, kwa kuongeza elimu yake Nje na kurudi nchini.Tunamshauri atumie elimu hiyo
aliyoipata kuweka heshima ya TASNIA yetu badala ya kuidhalilisha kwa kuandika
habari zisizo, ATTRIBUTIO, BALANCE,TRUTH –Sisi
tunadhani anaweza kulisaidia gazeti lake ambalo KITAALUMA kwa sasa linajitambilisha kwa pwaya halizingatii
MAADILI .
(YEYOTE YULE MWENYE
HOJA NASI TUNAYOSEMA AITE JOPO TUYACHAMBUE KISOMI KWA FAIDA YA WATANZANIA)
HAMZA KONDO
RAIS CHAMA CHA
WAANDISHI WA HABARI TANZANIA
(TAJA)
MWANACHUO WA SHAHADA YA UZAMIVU MAWASILIANO YA UMMA(PhD in Mass
Communication) OUT.-mwaka wa tatu.
Mob: 0786450000.
CC-Mitandao ya Jamii
na vyuo vikuu.
No comments:
Post a Comment