Kwa
nyakati fofauti, wengi wetu tumejifunza katika historia ya nchi yetu
kwamba moja ya sababu za msingi ambazo Mwalimu Nyerere alizitaja miaka
50 iliyopita kwamba ni kikwazo kwa Maendeleo ya taifa letu ni uhaba wa
wataalam wa kusaidia kujenga taifa. Hivyo, katika miaka ya mwanzo ya
uhuru, ilimlazimu Mwalimu na serikali yake kuagiza wataalam kutoka nje
na hawa walikuwa wanalipwa na fedha za walipa kodi wa nchi yetu. Miaka
50 baadae, hali sio tofauti sana kwa maana ya kwamba bado kama taifa,
hatuoni bado mchango wa kutosha kutoka kwa wataalam wetu katika
kuendeleza nchi yetu. Tunabaki kujiuliza, tatizo ni nini hasa: · Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum? · Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)? ·
Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic
institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao
kuchangia ujenzi wa taifa? · Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi? · Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa? Nia
yangu sio kutoa majibu kwa maswali haya bali kuchokoza mada huku
nikijaribu kutoa maoni yangu kadhaa juu ya jambo hili. Kwa sasa
nitajikita zaidi kwenye kujenga hoja kwamba moja ya tatizo lililopo ni
kwamba wasomi/watalaamu wetu wengi wamegeuka kuwa wanasiasa. Katika mazingira yetu, tunapozungumzia Siasa,
ni vigumu kutenganisha neno hili na dhana ya Siasa ya Vyama. Kwa maana
nyingine, in Tanzania, politics is partisan politics. By tradition,
vyama vya siasa uhakisi na kukimu zaidi matakwa na mahitaji ya watawala
kuliko matakwa na mahitaji ya jamii. Ni jambo la kawaida kwa vyama vya
siasa kutumia muda mchache sana kujishughulisha na matatizo/changamoto
zinazokabili jamii na badala yake kujikita katika masuala yanayohusiana
na uongozi na kutwaa madaraka. Suala hili linapotokea kwenye jamii
maskini kama Tanzania, jamii ambayo hakuna mjadala kwamba haina Dira ya
Maendeleo inayoeleweka kitaifa, hili ni tatizo. Kwa mfano, ukimuuliza
mtanzania wa kawaida kwamba, je dira ya taifa lako ni nini? Wengi
watakujibu kwamba dira yetu ni MKUKUTA au MKURABITA. Ni watanzania
wachache ambao watatamka “DIRA 2020” – na hata hivyo, huu ni upuuzi
kwani Dira hii haikutengenezwa na watanzania bali wahisani kupitia IMF
na World Bank. Kwahiyo sio Dira inayotokana na watanzania. Lakini mbaya
zaidi ni kwamba, katika kujibu swali juu ya dira yetu ya taifa,
watanzania wengi watakujibu kisiasa zaidi kwani huo ndio ufahamu wa
wengi – yani katika mazingira ya ilani za vyama vyao vya siasa. Huu ni
ujenzi wa janga kubwa sana la kitaifa kwa siku za usoni.
Kwa mtazamo wangu, ni muhimu katika mijadala juu ya Maendeleo ya Taifa,
tukaanza kupunguza siasa za vyama kwani inazidi kutugharimu kimaendeleo.
Ni muhimu tukaanza kujadili na kupangiaa Maendeleo ya Taifa letu katika
mazingira ambayo ni over and above partisan politics. Mimi nadhani
wenye uwezo wa kutufikisha huko ni wasomi (ambao ntawaita -
intellectuals). Kabla sijaenda mbali, ni vizuri nikafafanua an
intellectual ni mtu wa namna gani: An intellectual ni mtu anaetumia
akili yake kwa ubunifu, lakini muhimu zaidi mtu anaetumia intelligence
zaidi kuliko emotions or instincts. Hapa, maana ya intelligence ni –
uwezo wa kuchanganua, kutambua, na kuelewa jambo. Na na ndio maana
intellectuals katika jamii yoyote ile wana uwezo mkubwa wa kuona masuala
mbali mbali over and above partisan politics, hawa yale yenye maslahi
kitaifa.
Tofauti na miaka ya nyuma, Tanzania ya leo imejaliwa kuwa na wasomi
wengi sana waliotokana na vyuo vyetu vikuu (ukiachilia wale
waliosomeshwa na walipa kodi nje ya nchi). Vyuo vikuu ni taasisi zenye
umuhimu wa kipekee wa kupangilia na kuendeleza a body of intellectual
thought, kitu amhacho jamii inaweza kuakisi. This body of intellectual
thought is supposed to be over and above mambo ambayo ni
dhahiri/yanayoonekana/eleweka kwa urahisi. Jamii kama jamii hutingwa na
many complex issues; na tatizo ukua zaidi wanasiasa wanapoingiza siasa
katika complexity iliyopo tayari ndani ya jamii; kitendo hiki huzidi
kuwagharimu na kuwaumiza watanzania kimaendeleo. Lakini kwa vile wasomi
wana nafasi na uwezo wa kushughulika na masuala mbalimbali ya kijamii in
a manner ambayo ni over and above partisan politics, hawa ndio wenye
jukumu kubwa la kuisaidia jamii yetu iondokane na miaka 50 ya umaskini
ambao kwa mshangao mkubwa na bila aibu, CCM imeutungia kauli mbiu ya
Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele.
An intellectual body ni kama kioo cha jamii – kwa maana ya kwamba inaipa
jamii taswira yake. Wasomi wa nyanja mbali mbali (politics, law,
geology, engineers, journalism, medicine etc) wana uwezo na wajibu wa
kutuelezea watanzania tunaonekana vipi kama jamii. Wasomi wana uwezo na
wajibu pia to ‘articulate’ our hopes and fears; kutupa tahadhari juu ya
hatari iliyopo mbele yetu; na vile vile kutusaidia kutupatia maana ya
vitu ambavyo wanasiasa wetu aidha wanavipotosha, hawavielewi au
wanafanyia mzaa kwa faida zao binafsi.
Ninapoizungumzia zaidi CCM ni kwa sababu hadi sasa, ni chama pekee
ambacho miaka nenda miaka rudi (kwa miaka 50), ndicho kilichopewa
dhamana ya kutuongozi kama taifa. Hivyo ni muhimu nikajadili aina ya
viongozi wa CCM ya leo kwa mujibu wa maoni yangu. CCM in aina kuu tatu
ya viongozi wa kisiasa:
1. Wanaitikadi Feki: Wanaitikadi wa dhati CCM hawapo tena kwani
waliondoka na Mwalimu Nyerere. Wanaitikadi wa leo ni wale wajipambanua
kama wana itikadi wa kijamaa, lakini wanadanganya wananchi huku
wakitambua wazi kwamba CCM hakikuwaandaa watanzania kuhamia kwenye mfumo
wa soko huria kutoka kwenye ule wa awali wa Ujamaa. Ndio maana
watanzania wengi leo hii wamebakia kuduwaa na wasijue jinsi gani ya
kukabiliana na maumivu ya sera za soko huria huku viongozi wanaohimiza
CCM ni chama cha kijamaa wakiishi maisha ya ubepari uliopitiliza. Ni
wajibu wa wasomi kurekebisha hili, sio wanasiasa.
2. Wapambe: Hili ni kundi la pili la viongozi wa kisiasa ndani ya
CCM ya leo. Enzi za uchifu, hii ilikuwa ni ajira rasmi. Lakini leo hii,
watu huteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali lakini unofficially, kazi
yao ni upambe ambapo shughuli yao kubwa huwa ni to ‘amuse’, ‘cheer’ and
‘charm’ their masters (waliowapa madaraka). Hivyo ndivyo wanavyofanikiwa
kuhudumia matumbo yao na familia zao. Mbali na kufanya shughuli zao
kupitia vyombo vya habari, wapambe wapo hata ndani ya bunge, CCM – NEC
na kamati kuu ambapo kazi yao kubwa ni kuwafagilia wakubwa waliowapa
madaraka au fadhili kampeni zao, lakini muhimu zaidi, kusaidia CCM to
divert attention ya umma from major issues of the day. Wapambe ni nuksi
na kama msomi, ukikwaruzana nao, ni rahisi sana kukumaliza kibiashara,
career-wise na hata kimaisha.
3. Wachochezi (Political trouble makers) – kundi la tatu ni lile
la wachochezi. Kazi kubwa ya watu hawa ni kuushawishi na ku-bamboozle
umma, na ni mabingwa wa kutumia vyema prejudices na stereotypes zilizopo
kwenye jamii yetu kwa maslahi ya CCM. Viongozi hawa huwa hawaheshimu
mantiki (logic), human decency, consistency na hawana muda kusoma alama
za nyakati. Misamiati na kauli mbiu nyingi za CCM hutokana na viongozi
wa namna hii wakisaidiwa na wenzao (wapambe na wanaitikadi feki). Lakini
muhimu zaidi ni kwamba, hawa ni mabingwa wa kupika uongo mbalimbali
kisha kuujengea hoja na propaganda kwamba huo ndio ukweli uliosadidika,
usiopingika na unaotakiwa kuabudiwa. Na iwapo anatokea mtu mwingine
kupingana nao, basi ubatizwa kila aina ya majina – muhasi, haramia,
adui, mhuni, mkabila, n.k, na mara nyingine maisha yako yanaweza kuwa
hatarini. Wachochezi hawana muda wa kuheshimu dhana ya uhuru wa mawazo;
huwa hawaoni any merit on a political opponent (mfano tazama tabia na
kauli zao dhidi ya upinzani bungeni) na badala yake wanajaribu
kuwatuhumu wale wote wanaowa ‘challenge’ kwa mbinu za udini, ukabila,
ukanda, n.k. Viongozi wa namna hii ni mabingwa wa ku-appeal on
stereotypes, prejudices, emotions, fears, na expectations za umma kwa
kujenga propaganda based on themes za kidini, kikabila, ukanda n.k.
Wachochezi ndio hutumika zaidi katika kuzima hoja za wasomi zinazolenga
maslahi ya taifa.
Nini nafasi ya wasomi?
Tofauti na viongozi niliowajadili, kwa kawaida wasomi huwa ni ‘great
thinkers’. Tofauti kubwa iliyopo kati ya wasomi na viongozi
niliowajadili ni kwamba, wakati wanaitikadi feki, wachochezi na wapambe
ni kawaida kujichukulia madaraka mikononi kuifanyia jamii maamuzi,
wasomi wajibu wao ni kusaidia wananchi kujenga uwezo “to think for
themselves”. Ni tofauti hii kubwa baina ya viongozi hawa na wasomi ndio
inayofanya viongozi wengi wa kisiasa kuwapiga vita wasomi kila
wanapojitokeza kutoa maoni yao kuhusu muhstakabali wa taifa letu. Na
mbaya zaidi ni kwamba, sehemu kubwa ya jamii bado inaamini wanasiasa na
kuliko wasomi.
Kwa viongozi wa kisiasa, wasomi ni watu wabaya na wa hatari sana. Hii ni
tofauti na enzi za Mwalimu Nyerere kwani miaka ya 1960s – 1970s, kila
wakati taifa lilipokuwa linakabiliwa na changamoto mbalimbali, Mwalimu
alikuwa na utamaduni wa kwenda Chuo Kikuu (Mlimani) kukutana na
kujadiliana na wanafunzi. Ndio maana tofauti na leo, ilikuwa ni mara
chache sana kwa serikali ya Mwalimu kukwaruzana na wasomi. Moja ya
matukio machache ni lile la kuwalazimisha wasomi kujiunga na JKT ambapo
Samuel Sitta na wengine walijikuta katika matatizo pale walipopinga na
Mwalimu juu ya hilo. Kwa ufupi, enzi za Mwalimu, Mlimani became “a
symbol of expression of critical intellectual thought”. Tofauti na enzi
za Mwalimu, leo hii hatusikii wasomi wakishirikishwa na serikali katika
mijadala na maamuzi ya kujenga taifa letu. Na ni nadra sana kusikia
viongozi wa CCM wametembelea vyuo vikuu kwenda kubadilishana mawazo na
wasomi. Ni kama vile wanawaogopa na hakuna jamii hata moja duniani
iliyopiga hatua kimaendeleo kwa kuwaogopa au kutofautiana na wasomi.
Katika Tanzania ya leo ni vigumu sana kuyasikia mawazo ya wasomi.
Ikitokea bahati basi ni kupitia vipindi vya televisheni ambavyo sio
watanzania wengi wanapata nafasi ya kuvitazama, let alone kujua in
advance vipindi vitarushwa lini. Lakini mbaya zaidi ni kwamba hata
mawazo na michango ya wasomi hawa huishia kuwa soga tu kwani ushauri wao
haufanyiwi kazi yoyote na serikali.
Ni desturi pia kwa viongozi wengi wa kisiasa (CCM) kujenga hoja (chini
kwa chini) kwamba wasomi ni watu ambao wapo too academic, too
theoretical; wasomi hawaelewi reality; wasomi ni arm chair critics na
wamejaa destructive criticisms. Hoja hizi ni za kawaida hasa nyakati za
chaguzi mbalimbali za CCM. Kwa mfano, mwaka 2005 kulikuwa na fitina
nyingi sana kwamba mgombea – Professor Mwandosya hafai kuwa Rais kwani
Tanzania haina mahitaji na Rais ambae ni professor. Hata katika nafasi
za ubunge na udiwani, wasomi hujengewa chuki na fitina kubwa. Lakini
viongozi hawa hawa wa kisiasa baadae hushangaza pale wanapopigana
vikumbo kutafuta degree za kuchakachua, huku wengine wakitafuta degree
za PhD kwa kila njia ili na wao waonekana wa maana mbele ya jamii.
Tukirudi kwenye hoja kwamba wasomi hawafai kwani ni watu waliojaa theory
pekee, as a matter of fact, kwa msomi wa kweli na alie makini,kuitwa
too theoretical sio matusi kwani kazi kubwa ya msomi is to theorize
reality na hivyo ndivyo msomii uzidi kuelewa ukweli wa suala husika.
Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba - Wanasiasa wa CCM wanaposema wasomi
kazi yao kubwa ni ‘destructive criticisms’, na sio ‘constructive
criticisms’, wanacho maanisha hapa ni kwamba: Yale yote ambayo wanasiasa
hawa au CCM hawataki kuyasikia au hawataki wananchi wayaelewe, basi
hayo yote ni desctructive; Lakini yale yote ambayo wao au CCM inayaunga
mkono, yale ambayo hayakiweki CCM katika hatari ya kuanguka kisiasa, na
hayasaidii kuamsha watanzania kutoka kwenye usingizi mzito wa miaka 50
ya umaskini, basi hayo yote ni constructive. Isitoshe, ni dhahiri kwamba
katika Tanzania ya leo, hakuna msomi makini ambae anaweza kujenga hoja
na asionekana hafai machoni mwa CCM. Kwa mfano, zipo taarifa zisizo
rasmi kwamba hata ndani ya vikao vya baraza la mawaziri, wapo mawaziri
kadhaa ambao uonekana na mawaziri wenzao kwamba wanachafua hali ya hewa
kutokana na hoja zao kulenga zaidi maslahi ya taifa - over and above
partisan politics.
In actual fact, constructive criticism ni ile inayolenga kuondokana na
existing dominant, unfair, unjust and unequitable relationship ndani ya
jamii yetu ya Tanzania chini ya utawala wa miaka 50 wa CCM. Ndio maana
it turns out kwamba any serious criticism ya wasomi ni Destructive kwani
- such criticism uhimiza the need to Construct a new Tanzania. Kwa
mfano, watanzania wamepitia tabu kubwa sana kutafuta katiba mpya ambapo
kwa miaka mingi wasomi wamepigana kufa na kupona na utawala wa CCM
(kihoja) na hatimaye kupata ushindi dhidi ya CCM. Ni muhimu kwa wasomi
kuendeleza juhudi za aina hii kwani mbali ya suala la katiba Mpya ambalo
dhahiri ni non-partisan, yapo mengine mengi ambayo wasomi wanaweza
kusaidia ili watanzania wapigie hatua kimaendeleo.
Last edited by Mchambuzi; 22nd July 2012 at 21:15.(CHANZO : JAMII FORUMS)
|
No comments:
Post a Comment