Mama salma kikwete tukumbuke wenzio
Kwako Mama Kikwete, Saalam, Pole
kwa majukumu mengi uliyonayo mimi binafsi nakutakia mfungo mwema wa
Ramadhan na nina imani mwezi huu utakua na manufaa mengi kwako na kwetu
kwa ujumla MAANA UTATUOMBEA WALIMU WENZIO.
Pamoja
na salamu hizi napenda nieleze wazi kuwa mzee alipata kura nyingi zetu
walimu kutokana na wewe, ndo maana tulidiriki kumwita shemeji yetu,
tuliamini urais kuwa kwake utakua kwako pia na hatimae kwetu walimu
wenzio. Tulijua tuna mtu wa kutusemea sasa ambae ni wewe, Tulijua
unayajua vema maisha ya walimu wenzio na kwamba utapata muda wa
kumshauri baba kuhusu kundi hili ambalo wewe ulikua mdau kwa muda mrefu.
Mzee wakati wa kampeni mwaka 2005 nakumbuka alikua Mwanza alisema serikali yake itamaliza matatizo ya walimu nao wabaki
na kazi ya kusomesha watoto tu. lilikua jambo lililoibua hisia za
walimu wengi, na kwakweli tulikua tayari kufa na shemeji yetu. alishinda
vema naamini walimu wengi walitoa uungaji mkono nikiwemo na mimi.
Dada/mama taaluma hii bado ina hali mbaya maisha yetu yamejaa mashaka,
tumeshindwa kupata milo mitatu kwa siku, tumeshindwa sasa kulipa ada za
watoto wetu mashuleni, tumekopa kila pahala penye kukopesha ili tuweze
kupata ada za wanetu ambao wanaunyafuzi kutokana na milo duni
tunayoawalisha kutokana na uwezo wetu mdogo. Wapo wenzetu wanapata
mshahara sh 0/= kutokana na mazingira kama hayo niliyoeleza hapo juu!
Tumejaribu
kuyaeleza haya kwa muda mrefu bado hatujapata faraja wala nafuu, chama
chetu cha walimu kikajaribu kuhangaiika kuona kama tunawez kufikiriwa,
na hatimae tupate aheri. wameenda mahakamani hapakutokea mabadiliko,
ikabidi watangaze mgomo ambao kwakweli tulitamani mzee na wewe msikie
walimu wanamateso gani huku kwenye profession yako bado nako
tumechinjiwa baharini 1/8/2012
mzee akatoa hotuba nzuri sana ingawa ndani yake tuliona hukumu
itakauaje siku ya leo tarehe 2/8/2012, mama wakati tukisubiri hukumu
wengi walitubeza kuwa hukumu tayari imetolewa na mzee na mahakama
itatimiza unabii tu! Nikweli imekua hivyo.
Mama/dada
unaweza ukaona tunavyohangaika ili kupata nafuu ya maisha katika nchi
hii ambayo inaongozwa na mtu aliyeoa dada yetu itakuaje akija mtu ambae
hana kabisa uhusiano nasi? Natamani sana mwanangu au ndugu yangu
asijiingize kwenye taaluma hii maana haithaminiwi tena na wala
haionekani kama ina umhimu wowote.
Mama
kwani wakati mnapoongea na mzee kwa masuala ya kifamilia au ya kitaifa
huwezi kumshauri walau awe na huruma kwa kaka na dada zako sisi? Naamini
ukijipa assignment ya kufanya hivyo kila jioni utatuokoa na kwakweli
hata baada ya 2015 tutakukumbuka kwa kutupigania.
Mwisho
dada utakapokua kuwa ukila na kunywa hapo magogoni, ukumbuke wenzio
huku hata kuamkia mhogo au kiazi haiwezekani tena maana hata mvua
hazinyeshi vizuri hata mavuno hatupati kwenye vishamba vidogo
tunavyomudu kukodi vijijini, Utakapo
kuwa ukilala na kusinzia ukumbuke wenzio tunafukuzwa na wenye nyumba
kwa kukuchelewa kulipa pango la nyumba za udongo tulizopanga kutokana na
kutokuwepo kwa nyumba mashuleni. Aidha utakapo kuwa ukisafiri kwenye
ile ndege ndani au nje ya nchi, tukumbuke wenzio hata matairi ya
baiskeli zetu yameisha tunasubiri mshahara walau tununue mengine ili
tujiepushe na pancha za mara kwa mara.
ujapoita
watoto yatima na wanawake kuwafuturisha jioni hapo pembeni ya bahari
tukumbuke wenzio hatuna hata uwezo wa kutoa mchango wa rambirambi mtaani
ila tunakopa kila misiba inapotokea tukisubiri mwisho wa mwezi.
Mama/dada
najua unafahamu kuwa kile ambacho kingetupa kipato kidogo ni kuuza
ubuyu na barafu lakini tumezuwiwa na walimu wa kuu. Tumetii yote hayo
tumejaribu tuiition bado madiwani na wazazi wametushtaki. Tumeshindwa
kote sasa TUNAKUANGALIA WEWE TU. Tafadhali fanya haraka kumshauri mzee
vinginevyo utatukuta tumekufa kwa njaa, shinikizo la damu au utapiamlo.
Utakuta ndugu zako huku hatuna tumaini hata stori hatutakupa juu ya
maisha ualimu uliyoyaacha kwa miaka 10. Nakutakia maisha mema na utetezi mwema wa walimu wenzako.
Mwalimu Mpole |
No comments:
Post a Comment