Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega wilayani Magu, Dk. Raphael Chegeni,
Habari
zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Mbunge wa zamani wa
Jimbo la Busega, Wilayani Magu, Jijini Mwanza, Dkt. Raphael Chegeni,
'amelizwa' vitu vyake kadhaa ikiwamo na bastola yake.
Kwa
mujibu wa chanzo cha habari hizi, kinasema kuwa Dkt. Chegeni ameibiwa
usiku wa kuamkia leo, baada ya watu wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi, kuvunja Ofisi ya mheshimiwa huyo.
Aidha
imelezwa kuwa Majambazi hayo baada ya kuvunja mbali na kuchukua
Baastola hiyo, pia wameondoka na Kasha maalum la kuhifadhia Fedha pamoja
na Laptop iliyokuwa mezani.
Ikithibitisha
tukio hilo, polisi mkoani Mwanza, imesema wezi wamekomba sh. Milioni 5
za madafu na Dola 13 za Kimarekani zilizokuwa kwenye sefu hiyo.( KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO)
|
No comments:
Post a Comment