Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( taifa stars) wkifanya mazoezi ya mwisho mwisho kabla ya mechi yao dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya Ivory Coast itakayopigwa leo usiku. |
TIMU ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars), leo ina kibarua kigumu leo usiku cha kusaka ushindi dhidi ya Ivory Coast watakaokuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, jijini Abidjan katika mchezo wa kwanza kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.Mchezo wa leo unatarajia kuanza saa 11 jioni kwa saa za Ivory Coast na itakuwa ni saa mbili usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Stars iliyowasili Abidjan juzi jioni, inatazamia kupata kibarua kikali kutoka kwa Ivory Coast iliyokusanya mastaa wake wote wakali wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya wakiongozwa na Didier Drogba.
Stars ambayo kocha wake, Kim Poulsen anajivunia zaidi mshambuliaji wa kimataifa anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya TP mazembe, Mbwana Samata, jana jioni ilifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya pambano hilo katika uwanja Felix Houpheut Boigny. Pamoja na hayo yote kocha mkuu wa stars amesema hana wasiwasi sana na vijana wake na anatarajia kufanya mabadiliko kidogo katika kikosi kitakachoanza katika mechi ya leo.
No comments:
Post a Comment