Raisi wa Malawi Bi Joyce Banda |
Rais wa Malawi, Joyce Banda,
ameamua kuuza ndege ya rais pamoja na magari ya kifahari.Ndege hiyo ilinunuliwa
kwa dola milioni-13 na rais aliyemtangulia, Bingu wa Mutharika, aliyefariki
mwezi wa Aprili.Rais Banda amenukuliwa kusema kwamba anatosheka kusafiri kwenye
ndege za abiria kama watu wengine, kwa sababameshazowea kutembea kwa miguu na
kusaidiwa na wasafiri njiani.
Fedha zitazopatikana katika mauzo
ya ndege na magari hayo, zitatumiwa kuwasaidia maskini wa Malawi. Serikali
ya Uingereza, ambayo ndio mfadhili mkubwa wa koloni yake hiyo ya zamani,
imepokea vema uamuzi huo kuwa ni ishara inayotia moyo. ( kwa hisani ya MY TANZANIA BLOG)
No comments:
Post a Comment