DAWA
mpya inayokinga na kuua kwa kasi virusi vinavyosababisha ugonjwa wa
Ukimwi, tayari imeshaanza kutumika, hii ni kwa mujibu wa ripoti za
mitandaoni. Dawa
hiyo ambayo toleo lake la kwanza ipo kwenye muundo wa vidonge, inaitwa
Truvada na tayari imekwishaanza kufanya kazi nchini Marekani. Kitendo
cha Truvada kukubalika na Mamlaka ya Usimamizi wa Chakula na Dawa
nchini Marekani (FDA), kinatoa picha kuwa sasa vidonge hivyo vinaweza
kuuzwa sehemu yoyote duniani. Kamishna
wa FDA, Margaret Hamburg, amesifu Truvada na kueleza kwamba itapunguza
wastani wa maambukizi mapya pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa
Ukimwi. Hamburg
alisema kuwa hivi sasa nchini Marekani kumekuwa na kasi ya maambukizi
mapya, kwani kila mwaka kumekuwa na wastani wa watu 50,000 wanaobainika
kupata Virusi Vya Ukimwi (VVU). Watafiti
waliogundua Truvada wanaeleza kuwa dawa hiyo kwa sehemu kubwa inakinga
VVU na upande mwingine inasaidia kuua virusi vya Ukimwi kwa mtu ambaye
tayari amekwishaathirika. Hata
hivyo, FDA na watafiti hao, hawajaeleza kama Truvada inatibu moja kwa
moja, isipokuwa wanasisitiza: “Inamkinga mtu kupata maambukizi mapya,
inamsaidia mwathirika kwa kuua VVU pamoja na kumkinga dhidi ya magonjwa
nyemelezi.” |
No comments:
Post a Comment