FOLLOWERS

Friday, August 3, 2012

NANENANE DODOMA : WIZARA YA FEDHA YATOA ELIMU

Kaimu Afisa Uhusiano wa  wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Hawa Kikeke(kushoto) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia  Maafisa wa Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma

Mwanasheria kutoka  Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Emilia Mkubulo(kulia) akimwelimisha mmoja wa wananchi faida za kununua hisa  jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.

Mtunzaji Kumbukumbu na Mhasibu Abbas Mnyeto  wa Wizara ya  Fedha wakiwasaidia wazee wastafu upande wa Kilimo juu ya taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wanapostaafu jana mjini Dodoma walipokuwa kwenye banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane. 

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...