FOLLOWERS

Friday, August 3, 2012

MTU MMOJA AFARIKI MWANJELWA MBEYA BAADA YA KUNYWA SUPU

KATIKA hali ambayo si ya kawaida mwanaume mmoja ambaye hakutambulika jina wala mahala anakotokea mpaka tunakwenda mitamboni, amefariki dunia ghafla baada ya kile kinachodaia kuwa kifo chake kimetokea muda mfupi baada ya kunywa supu kisha kusubiri usafiri wa kuelekea Tukuyu.

Mashuhuda wa tukio hilo wameuambia mtandao wa kalulunga.blogspot.com kuwa mwanaume huyo alionekana maeneo ya stendi ya Mwanjelwa Jijini Mbeya akiwa anasubiri usafiri kisha akatoka na kwenda kunywa supu pembeni kidogo na alipomaliza alionekana akikosa nguvu kisha kuanguka na baada ya dakika kumi akabainika kuwa amefariki dunia.

Baada ya kuona hivyo, askari waliokuwa eneo hilo walipewa taarifa na kufanya utaratibu wa kuichukua maiti hiyo na kuipileka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Mbali na mwanaume huyo pia alionekana mwanaume mwingine ambaye alivalia mavazi ya assili ya kimasai naye akikosa nguvu na kuanguka lakini alipatiwa huduma ya kwanza na wenzake ambao alikuwa nao kwa kunyweshwa dawa za jadi kisha akaonekana kupata nguvu na kuondoka nmae eneo hilo.

Mpaka tunaenda mitamboni hakuna taarifa zozote za mtu kishikiliwa kutokana na Tukio hilo la kusikitisha ambapo tukio hilo limekuja miezi minne baada ya mwanamke mmoja kukimbia katika stendi kuu ya mabasi ya mkoa wa Mbeya baada ya kubainika kuwa chai aliyokuwa akiiuza kwa wateja wake ilikuwa ni damu. 
(KWA HISANI YA KALULUNGA COMMUNITY MEDIA)

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...