MKUTANO
Mkuu wa Wanachama Wote wa Simba utafanyika Agosti tano mwaka huu katika
Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay kama ilivyopangwa.
Mipango
yote kwa ajili ya mkutano huo muhimu kikatiba imekamilika na klabu
inawaomba wanachama wake wote hai kuhudhuria mkutano huo muhimu.
Uongozi
umepanga kutoa mabasi kwa ajili ya kuwasafirisha wanachama wake kutoka
katika maeneo mbalimbali kwenda katika ukumbi wa mikutano.
Kutakuwa
na mabasi matatu kwenye eneo la Shibam Magomeni... Mabasi matatu Temeke
mwisho na mabasi matatu katika makao makuu ya Simba SC Mtaa wa
Msimbazi.
Pia
klabu itapeleka mabasi mawili katika wilaya za Mkuranga na Kibaha kwa
ajili ya kuwaleta wanachama wake walio katika mkoa wa Pwani kuhudhuria
mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, amewahakikishia wanachama wa Simba
kwamba mkutano huo utaendeshwa kisasa na usalama umehakikishwa kwa
asilimia 100 kwa vile eneo la mkutano liko chini ya Jeshi la Polisi.
"Napenda
kuwahakikishia wanachama wote wa Simba kwamba mkutano huo utakuwa bora
na wote watakaokuja watafurahi na kujisikia fahari kuwa washabiki wa
klabu ya soka ya Simba. Kwa wale ambao wamepanga kuja kufanya vurugu
kwenye mkutano huo, klabu itaviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake,"
alisema.
|
No comments:
Post a Comment