FOLLOWERS

Thursday, August 2, 2012

MISRI : KUAPISHA SERIKALI MPYA

Rais Mursi na Waziri mkuu mpya Qandeel
Misri punde itatangaza rasmi baraza jipya la mawaziri na kuapishwa na Rais Mohammed Mursi, aliyeshika wadhifa wake mwezi uliopita.
Taarifa za vyombo vya habari vinaripoti kuwa serikali ya Waziri Mkuu Hisham Qandil itakuwa ya wataalamu zaidi ikiwa na angalau mawaziri wawili kutoka serikali iliyopita na Waislamu wachache.
Kiongozi wa zamani wa kijeshi Mohammed Hussein Tantawi anatarajiwa kuwa waziri wa Ulinzi.
Bw. Qandil ameshasema 'sifa ya uwajibikaji' itakuwa ni kigezo kikubwa cha kuteuliwa.
Akizungumza wiki iliyopita, alisema alitaka ''vikundi vyote vya kisiasa na watu wa Misri kutuunga mkono katika jukumu hili,' akigusia zaidi changamoto za kiuchumi na kijamii.
Rais Mohammed Mursi amekosolewa kwa kuchukua muda mrefu kutaja jina la Waziri Mkuu na kuunda serikali tangu ashike madaraka mwezi Juni.
Kumteua Bw Qandil, aliyekuwa waziri wa Maji kumewashangaza wengi ambao walikuwa wakitegemea jina maarufu.
Ikilinganishwa na mambo yanavyokwenda nchini Misri kipindi kilicho mbele yetu kitatulazimu sisi wote serikali na watu kupfanya kazi pamoja ili kuhakikisha kuna utulivu " alisema Ahmed Jamal al-Din Naibu Waziri wa mambo ya ndani
Jumatano vyombo vya habari vya umma vimeripoti kuwa Waziri Mkuu Mteule alimwambia Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed Kamal Amr na Waziri wa Fedha Mumtaz al-Said kuwa watabaki kwenye nafasi zao.
Maja Jenerali Gen Ahmed Jamal al-Din, Naibu Waziri wa Ulinzi amepewa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, vilifafanua.
"kutokana na hali inavyokwenda nchini hatuna budi kufanya kazi pamoja serikali na wananchi' Jenerali huyo aliwaambia waandishi wa habari mjini Cairo.
Maafisa pia walisema Field Marshal Mohammed Hussein Tantawi, mkuu wa Baraza kuu la Kijeshi atakuwa Waziri wa Ulinzi, pamoja na tamko la katiba ya mpito lililotolewa baada ya uchaguzi wa Rais mwezi Juni.
Baraza hilo Scaf lilichukua nafasi ya uongozi baada Hosni Mubarak kung'olewa madarakani mwezi FebruarI 2011.
Tamko na uamuzi wa kuvunja bunge siku chache baada ya kuchaguliwa lilileta hasira na kufunika makabidhiano ya madaraka ya Rais Mursi Juni 30.
Kati ya mawaziri 18 waliotajwa mpaka sasa kwa kupitia vyombo vya habair vya umma wawili ni kutoka chama cha Muslim Brotherhood (FJP), ambacho Bw Mursi alikuwa akikiongoza.
Mustafa Musaad, ambaye anahusika na sera za elimu wakati wa kampeni za uchaguzi atakuwa waziri wa Elimu, huku Tariq Wafiq, mkuu wa kamati ya makazi wa chama cha FJP atakuwa waziri wa makazi.
Nafasi nyingine muhimu, ya waziri wa masuala ya kidini (Awqaf), imechukuliwa na Osama al-Abd, Rais wa chuo kikuu cha al-Azhar .
Kumekuwa na tetesi kuwa kiongozi wa kundi la wahafidhina wa Ki-Salafist, Mohammed Yusri Ibrahim, naye atateuliwa.
CHANZO; www.bbcswahili.com

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...