Katika kuhakikisha kuwa tunakwenda na kasi ya teknologia inayoenda
kwa kasi duniani, Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) sasa kimeanza rasmi
kufundisha kwa kutumia mtandao na kuhakikisha
kila mhadhiri, anafundisha madenti wengi kwa wakati mmoja.
Hilo
liliwekwa wazi juzi na Balozi Juma Mwapachu, alipokuwa akizungumza na
wahadhiri wa Udom katika ufunguzi wa mafunzo ya ufundishaji kwa njia ya
teknolojia hiyo.
Mwapachu ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la
chuo hicho, alisema wingi wa wanafunzi katika chuo hicho kikubwa kwa
sasa hauendani na idadi ya wahadhiri waliopo na kwamba bila ya kuwa na
mbinu mbadala za kuwafundisha, wanafunzi wataachwa nyuma.
“Udom sio chuo cha kawaida katika nchi za Afrika Mashariki, lakini pia
niseme kuwa siyo vyuo vingi hapa duniani vimeweza kupata bahati ya
kukua kwa kasi kubwa ndani ya miaka minne kama Udom, kwa hiyo ukuaji wa
chuo hiki lazima uwe wa kisasa na unaokwenda na sayansi na teknolijia,”
alisema
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Udom, Prof Idris
Kikula, alisema chuo kilikuwa kinakabiliwa na tatizo katika
ufundishaji, hatua iliyoulazimisha uongozi kubuni mkakati huo.Kikula
alisema hatua ya sasa ni ya kuwajengea uwezo wahadhiri, ili waweze
kufanyakazi zao kwa ufanisi mkubwa zaidi. |
No comments:
Post a Comment