PRESS STATEMENT HOTUBA YA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TAIFA- SANGO GUNGU KASERA 2 August 20112 Ndg: Wanahabari Ndg: wana UVCCM wenzangu
Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kutoa salamu zangu za dhati
kwa Watanzania na vijana wenzangu wa nchi hii pamoja nanyi waandishi wa
Habari kwa kushiriki nami katika safari hii inayolenga kuunganisha na
kujenga hatua za mabadiliko ya maisha ya Vijana wa Tanzania.
Kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru na kuwaomba mshikamano vijana
wenzangu wa Chama cha Mapinduzi ambao kupitia kwao ninatumia nafasi hii
kuomba ridhaa yao ili nipate nafasi ya kuwa chemchem ya mafanikio na
mabadiliko katika maisha yetu kwa kuanzia na chama chetu.
Leo hii naungana na vijana wenzangu hawa wa ndani ya CCM, kufanya jambo
moja kubwa, jambo la kuchukua fomu ya kuwania moja ya nafasi kubwa
katika jumuiya ya Vijana wa CCM Tanzania. Ninafanya kazi hii leo
nikitambua mambo yafuatayo: Kwanza, ninalenga kuleta
mabadiliko yanayotazama aina ya vijana tuliopo sasa, aina ya maisha
tunayoishi na aina ya changanoto zinazotukabili mimi nikiwa mmojawapo.
Pili kwa upekee mkubwa, nachukua fomu hii nikibaini hali ya vijana huko
tulikotoka na, changamoto tulizopitia na hatari inayotukabili mbele
kama hatua stahiki hazitaanza kuchukuliwa na vijana wa aina yangu ambao
tuna uzoefu wa kutosha wa maisha ya kawaida ambayo yanahitaji nguvu na
akili zetu na za wenzetu waliotutangulia katika kuboresha maisha yetu
ili tuweze kuwa raia wema katika nchi yetu na wanachama waadilifu wa
chama chetu na jumuiya zake Ndugu Waandishi wa Habari;
Kazi hii ya kuchukua fomu ninayoifanya leo hii na kisha kuanza zoezi la
kutafuta kuungwa mkono.Ni kazi inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa
uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na vijana mbalimbali bila kujali itikadi
zao za vyama vya siasa. Nasema hivi kwa kutambua kuwa UVCCM
ndiyo Jumuiya pekee yenye kubeba taswira na matarajio ya vijana wa
Tanzania na ambayo siku zote inatakiwa kusimamia maslahi na matakwa ya
vijana wa Tanzania na kwa kuwa jumuhia hii ni jumuhia ya chama
kinachoongoza si chama tawala . Ndugu zangu wanahabari na wana
CCM tunafahamu tofauti kati ya kuongoza na kutawala ndio maana nimetumia
neno kuongoza ,na Kama kazi hii ilikuwa haifanyiki huko nyuma na kama
ilifanyika bila kuridhisha, mimi nimeamua kwa moyo mkunjufu kuingia
kuonesha namna jumuiya yetu itakavyoweza kuwatumikia vijana wa Tanzania
na kukiboresha chama cha Mapinduzi ili kitambue wajibu wake kwa vijana
wote wa Tanzania na kwa kufanya hivi kiweze kusimamia misingi
iliyolijenga Taifa hili na kuachwa na waasisi wa Taifa letu Hayati Baba
Wa Taifa na Hayati Rais Karume ambao walilijenga taifa letu katika
misingi ya haki, usawa na ustahimilivu. Ndugu wana habari;
Katika kipindi hiki cha kutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa
nafasi hii nitabakia kuongozwa na Moto isemayo: Vijana kwanza kwa taifa
lenye amani na maendeleo. Bila vijana kuangaliwa na kupewa yale
wanayostahiki, ni wazi taifa lenye amani na maendeleo halitakuwepo.
Natambua fika kuwa vijana wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa
hasa ile inayolenga kubaini ndoto ya maisha yao ya sasa na siku zijazo.
Naamini mimi ni mmoja wa vijana hawa ambaye pia ninahitaji kuona vijana
walio katika kilimo basi wanaweza kupata soko la mazao yao. Vijana
wabeba mikokoteni nao wanafanya kazi hiyo kwa miaka kadhaa na kisha
kuboresha ajira zao. Vijana wanaosoma basi wanahitimu vema na kupata
ajira wanazostahiki na pia walio makazini na waliopata nafasi za
kuongoza wanaonesha mfano wa kufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii ili
kuonesha kuwa vijana tunaweza na hatuwezi kuliangusha taifa.
Natambua haya ninayoyazungumza ni mambo magumu lakini pia natambua
yanahitaji mbinu nyingi ili kukabiliana nayo. Kwa sasa natumia nafasi
hii kukiomba Chama changu, kuiomba Jumuiya Yetu ya Vijana kutambua kuwa
nina dhamira, nina nia, nina sifa za kutosha, nina uwezo wa kufanya
majukumu haya ninayoyaomba na ninafahamu kazi za majukumu haya.
Tena nina rekodi katika umri wangu huu wa kufanya mambo ya kutukuka
ambayo rekodi yake inaweza kutazamwa pote nilipobahatika kutoa utumishi
wangu. Kwa namna isiyoonyesha kuyumba naomba kuwaeleza vijana
wenzangu kuwa kutokana na mshikamano wa vijana wenzangu kwangu ni wazi
tumejiandaa kushinda katika nafasi hii ili tuweze kuleta mwanga wa
mabadiliko katika jumuiya yetu na chama chetu katika maandalizi ya
chaguzi zijazo. Ndugu wanahabari ninatambua zipo changamoto
nyingi zinazoikabili UVCCM na changamoto hizi zinahitaji kiongozi
ambaye atakuwa na uthubutu wa kuweza kukabiliana nazo,changamoto kuu ni
kitaswira, kimuundo, kiimani, kimadhumuni kama ambavyo zimehainishwa
kwenye kanuni za ummoja wa vijana. Nina maanisha nini
ninapozungumzia taswira ya UVCCM.Taswira ya UVCCM Taifa leo sio taswira
ya kimapambano.Historia yetu ipo wazi jumuiya ya vijana ilishiriki
katika mapambano ya kuleta Uhuru ,Umoja na mshikamano mtakumbuka wakati
TANU Inahangaika na kutafuta Uhuru wa Tanganyika na Afro-Shirazi party
ikipambana kuleta Uhuru wa Zanzibar vijana waliunganishwa na jumuiya za
umoja wa vijana wa vyama hivi viwili ambavyo ni TANU YOUTH LEAGUE na
ASP YOUTH LEAGUE,zinafahamika kazi zilizofanywa na wabeba mizigo wa
kariakoo mfano Mzee Rajabu Diwani, leo UVCCM sio tena ya wabeba mizigo ,
sio tena ya wamachinga sio tena ya wakulima ,sio tena jumuiya ya
wafanyakazi ni jumuiya ya wafanyabiashara, watoto wa
vigogo ama wenye nasaba nao ama rafiki zao,inahitaji viongozi wenye
dhamira ya dhati ambao watarudisha jumuiya hii kwa vijana wa kitanzania
na kurudisha taswira ya kimapambano ambayo ni mapambano ya kiuchumi,
kazi ya Uhuru imeshafanyika imebakia jukumu la kuleta Uhuru wa kiuchumi
na kuwa kimbilio la vijana wote.Ni dhamira yangu ya kugombea nafasi
hii ni kuhakikisha awamu ya pili ya mapambano ya kiuchumi ya umoja wa
vijana inaanza rasmi . Nafahamu zipo changamoto za
kiutawala,kiuchumi na jumuiya kuendelea kuishi kwa kutegemea misaada na
Ruzuku kutoka kwenye chama,nafahamu watendaji wana hali mbaya kiuchumi
hasa katika mawilaya ,nafahamu ofisi zetu za wilaya zina upungufu wa
vitendea kazi ni dhamira yangu kubadili mwelekeo wa utendaji wa jumuiya
yetu kutoka “Business as usual” kuvalisha skafu viongozi na kuimba
nyimbo ,kuwa jumuiya yenye dira na mwelekeo sahii wa kuwaunganisha na
kumkomboa kijana wa kitanzania Ndugu waandishi wa Habari;
Ninafahamu matarajio ya vijana wa kitanzania yatafikiwa kupitia CCM
imara na CCM inatokana na uimara wa jumuiya zake kuwa imara na ili
inawezekana kwa kupatikana viongozi Imara na mimi nina amini ni mmoja wa
viongozi ambao wataifanya jumuiya yetu kuwa Imara. Kwa
kuhitimisha Hotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu
kwa kunifanikisha kuwa nanyi hapa, niwashukuru wana familia yangu,
marafiki na nyie ndugu zangu waandishi wa Habari kwa kukubali kujumuika
nami kunisikiliza leo. Niwaombe Vijana wenzangu wa CCM kuniunga
mkono katika azma hii kubwa niliyonayo na niwakumbushe tu kuwa, zoezi
hili la kuchukua fomu nililofanya hapa leo si langu bali la vijana wote
wa Tanzania wakiwakilishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
Ni imani yangu kuwa, wana UVCCM hawatakubali kuangusha taa hii
waliyoiwasha kule Rorya mkoa wa Mara wao wenyewe na badala yake
wataungana nami bega kwa bega ili kuufikia ushindi.
Tutapitisha fomu hii pamoja nao, tutachujwa pamoja nao na kisha
tutashinda pamoja nao na kisha kuanza kuwaongoza vijana wa Tanzania
pamoja nao. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma atubariki na kutupa nguvu
tufanikishe azma hii muhimu pamoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi Asanteni kwa kunisikiliza. Mimi Ndg Sango Gungu Kasera- Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM (W) Rorya Kauli mbiu Mbiu “Vijana kwanza kwa taifa lenye amani na maendeleo’’.
|
No comments:
Post a Comment