Bodi
ya Taifa ya mashindano ya Miss Utalii,ktika kutekeleza mkakati wake wa
kujiimarisha na kujipanga kwa ajili ya mpango mkakati mpya wa muda
mfupi na muda mrefu wa miaka mitano na wa miaka kumi,imethibitisha
waandaaki wa mashindano hayo katika mikoa na kanda 17, huku ikitangaza nafasi
za wandaaji katika mikoaa na kanda mbalimbali Tanzania bara na
Tanzania Visiwani. Katika kupitisha makampuni na majina ya waandaaji hao
wa ngazi za mikoa, bodi imezingatia uwezo ,umakini na uwepo wa ofisi
na waandaaji katika wilaya,mikoa na kanda husika. Pia bodi imezingatia
kuwa na waandaaji makini ambao wanaweza kuendana na mfumi mpya wa
kitaasisi wa mashindano haya, mfumo ambao unatoa fulsa ya mgawanyo wa
madaraka na uwajibikaji wa pamoja na kila mmoja katika ngazi yake.
“
Bodi sasa imeamua kujenga taasisi imara ya kiheshimika na kukubalika
kitaifa na kimataifa,ni wakati sahihi sasa kwa mashindano haya kuchukua
nafasi yake ya kuwa shindano bora na kubwa kuliko yote nchini,Afrika na
duniani kwa ujumla, na hili litawezekana tu kwa kuwa na taasisi imara
na makini iliyojengwa na watu na makampuni makini. Wale waandaaji
wababaishaji,mamluki na wahuni sasa Miss utalii Tanzania sio mahala
pake”. Aidha bodi imewataka wasandaaji wote kukamilisha taratibu na
matakwa ya kanuni na taratibu za mashindano haya,kabla ya kufanya kwa
mashindano ya ngazi zao,ikiwemo kwenda kujitambulisha na kuchukua vibali
vya maafisa utamaduni. Aidha bodi imewaomba maafisa utamaduni wa ngazi
zote kutotoa vibadi kwa waandaaji hao kabla ya kukamilisha taratibu
iliwemo kukabidhi zawadi za washindi na washiriki siku saba kabla ya
tarehe za shindano husika. Mikoa na kanda hizo na majina ya waandaaki
katika mabano ni Arusha,Mara na Kanda ya Kaskazini ( NAman LIMITED
COMPANY LTD), Kilimanjaro na Manyara (NEW VISION PLAN COMPANY
LTD),Kagera ( FIOONA FASHION Limited) Mbeya ( WABUNIFU ENTERTAINMENT),
katavi ( KATABI COMPANY LIMITED), Dar es Salaam,Kinondoni,Ilala na
Temeke ( Tanzania Film Directors Association (TAFIDA)) Vyuo Vikuu Dar es
Salaam (Eriado Point View) ,Iringa na Kanda ya Kusini (DELIMA Hotel
& Tourism School),Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki ( L.J MEDIA
COMPANY), Mwanza (Fania Beauty and Salon Company). Mikoa ambayo
haijapata waandaaji baada ya maombi ya waliotuma kutikuwa na sifa, hivyo
wenye sifa wajitokeze kuomba kuandaa ni : Njombe, Pwani, Lindi,
Mtwara, Tanga Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita,
Tabora, Rukwa, Kigoma, Kanda ya Kati, Kanda ya Mashariki, Zanzibar,
Kanda ya Kusini Nyanda ya Juu, Kanda ya Magharibi, ,Vyuo Vikuu
Kusini,Vyuo Vikuu kaskazini,Vyuo Vikuu Magharibi,Vyuo Vukuu Kati,na
Vyuo Vikuu. Makampuni na watu wanaotaka kuandaa mashindano haya ya Miss
Utalii Tanzania wawasiliane nasi kupitia barua pepe
|
No comments:
Post a Comment