|
Bango lenye ujumbe wa kukataa kuwepo kwa geti la ushuru likiwa limewekwa barabarani na wananchi |
|
Sehemu ya uharibifu iliyotokana na maandamano ya wananchi kupinga uwepo wa geti la ushuru |
|
Barabara ikiwa imefungwa na wananchi kupinga uwepo wa geti la ushuru katika kijiji cha Ndaga wilayani Rungwe Mkoani Mbeya |
Wananchi wa kijiji cha Ndaga, wilayani Rungwe mkoani Mbeya hivi leo wamefunga barabara ya Mbeya - Rungwe kwa zaidi ya saa nne kwa madai kuwa hawalihitaji geti la ushuru wa mazao katika eneo lao kwa kile walichodai kuwa hawaoni faida yake kwani limejaa rushwa. wananchi wamevunja geti hilo na kuchoma moto nyumba iliyokuwa ikitumika kukusanya ushuru huo ( KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG)
No comments:
Post a Comment