Mheshimiwa Joseph Osmond Mbilinyi aka Mr II ( Sugu) ambaye ni mbunge wa Mbeya mjini akiwa sambamba na Fredy Malick ambaye pia ni katibu wake wakifanya shoo ndani ya ukumbi wa Dar Live DSM |
Mr II aka Sugu alifanya makamuzi ndani ya Dar Live Mbagala Jijini DSM |
Mbunge wa Mbeya mjini mheshimiwa Joseph Mbilinyi aka Sugu kwa tiketi ya CHADEMA wiendi hii alifanya shoo bab kubwa katika ukumbi wa Dar Live uliopo mbagala jijini DSM na kukonga mioyo ya mashabiki waliofurika ukumbini humo.
Mr II pia aliahidi kuwa shilingi milioni 2 kati ya milioni tatu atakazolipwa katika shoo hiyo atazipeleka kuchangia mfuko wa elimu katika jimbo la Mbeya mjini. katika shoo hiyo mr II alisindikizwa na wasanii wengine maarufu kama Mkoloni, Profesa J, Juma Nature na Vinega wote.
No comments:
Post a Comment