Raisi Mwai Kibaki wa Kenya na Waziri mkuu wa Kenye Raila Odinga |
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
ameomba msaada kifedha na vikosi kutoka Marekani na Ulaya kuwatoa al-Shabab kwa
‘shambulio la mwisho’ katika mji wenye bandari wa Kismayo.Raila Odinga alisema
vikosi vyaKenya vinatarajia kuingia Kismayo mwezi Agosti na alisema al-Shabab
itahitaji "operesheni ya kivita ardhini, baharini na angani".Lakini
msemaji wa sera za nje wa Muungano wa Ulaya Michael Mann alisema hiyo ni kwenda
kinyume na majukumu yake.Manowari za kivita zimekuwa katika eneo hilo tangu
mwaka 2008 kupambana na maharamia.Majukumu yake hivi karibuni yaliongezeka ili
kuruhusu mashambulizi ya ardhini dhidi maharamia wa Kisomali.Hadi manowari kumi
za kivita zinafanya doria katika Pembe ya Afrika kama sehemu ya harakati ya
Muungano wa Ulaya ‘Atalanta’ ambayo ilianzishwa kulinda biashara za bandarini
dhidi ya mashambulizi ya maharamia.
Lakini Bw Mann aliiambia BBC: "Hatuna
budi kuwa makini sana
kufanya harakati zetu katika mzingo wa sheria za kimataifa. Tunawajibika katika
jukumu letu ambalo ni kupambana na maharamia baharini kwa kuharibu mgome zao. "Iwapo
tutabadili hilo tutahitaji nchi wanachama 27
kukubaliana na hilo.
Kwa sasa tunaona kuwa kupambana na al-Shabab kwa ufanisi zaidi hakuna budi
kufanywe kwa namna nyingine"
'Kuwamaliza al-Shabab'
Askari wa Umoja wa Afrika, vikosi vya
Ethipia na vile vya serikali ya mpito yaSomalia katika miezi ya karibuni
yamefanikiwa kuwaondoa al-shabab katika miji kadhaa.Vikosi vya Kenya viliingia
Somalia mwezi Oktaba mwaka jana na taratibu vinasogea kuelekea Kismayo.Kismayo
kimsingi inachukuliwa kama mji muhimu wapiganaji wa al-Shabab kwa sababu
wanaudhibiti kupata fedha kutokana na mapato na kodi katika bandari hiyo.
No comments:
Post a Comment