FOLLOWERS

Monday, June 25, 2012

CCM WASITISHA MKUTANO WA KUHUSU UAMSHO

Makam mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, amesitisha mkutano wa hadhara uliyokuwa ufanyike jana kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar kufuatia kuibuka kundi la watu wanaotaka Zanzibar kujitega na Muungano.

Kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika mfumo wa muungano zimekuwa zikifanywa misikitini kwa zaidi ya miezi mitano na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya dini ya kislamu Zanzibar (Jumiki).

Kwa mujibu wa Uchunguzi wa NIPASHE, Mkutano huo, ulikuwa ufanyike katika viwanja vya Maisara Mkoa wa mjini Magharibi na kuhutubiwa na wanasiasa wakongwe Zanzibar akiwemo Rais mstaafu, wa Jamhuri ya Muungano, Ali Hassan Mwinyi.

Imedaiwa kwamba mkutano huo ulipangwa kufanyika baada ya kutokea shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi CCM mikoa ya Zanzibar nawanachama ambao wanataka msimamo wa Chama juu ya kikundi cha Uamsho ambacho kinaendelea na kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika wa Muungano.

Aidha, mkutano huo mbali na kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar, pia ungezungumzia mchakato wa katiba mpya na mafanikio yaliyopatikana ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010.

“Mkutano uliyokuwa ufanyike kuwajibu Uamsho wanaotaka Zanzibar kujitenga umesitishwa na Makamu Mwenyekiti Dk. Amani Karume,” alisema Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM Zanzibar.

Mkutano huo ambao ulipewa jina la “Mkutano wa kumtoa Paka katika Gunia” hulikuwa uhudhuriwe na wanachama wa CCM kutoka mikoa ya Zanzibar.

Mkutano huo uliandaliwa siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Haji Juma Haji, kulalamika kwa nini waasisi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Zanzibar (SUK) Dk. Karume na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, kukaa kimya tangu Uamsho kuanza kampeni za kutaka Zanzibar kujitega katika Muungano na kusababisha hali ya kisiasa kuchafuka pamoja na makanisa na baa kuchomwa moto.

Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu (NEC)  Idara ya Itikadi na Uenezi, Issa Haji Gavu, alithibitisha mkutano huo kuhairishwa kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo ikiwemo kujitokeza dharura kwa viongonzi waliotarajiwa kuhutubia mkutano huo.

Jumuiya ya Uamsho ambayo inaendelea na kampeni za kutaka kuitishwa kura ya  maoni ili wananchi waulizwe wanautaka Muungano. (CHANZO NIPASHE)

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...