Dk Harison Mwakyembe, waziri wa uchukuzi |
Wabunge wajumbe wa kamati ya miundo mbinu wamekwamisha kupitisha bajeti ya wizara ya uchukuzi kwa kile kilichodaiwa utekelezaji hafifu wa bajeti iliyopitishwa katika mwaka wa fedha 2011-2012 dhidi ya wizara hiyo. Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya kamati hiyo zinaeleza katika
kikao cha juzi, baadhi ya wajumbe walisema hawawezi kupitisha bajeti
hiyo mpaka wapate maelezo kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu
kutokutekelezwa kwa bajeti ya 2011/2012 ili wajue bajeti ijayo
itatekelezwa vipi.
No comments:
Post a Comment