Mshambulia wa Simba Emmanuel Okwi akishangilia moja ya magoli aliyoifungia timu hiyo |
Haruna Niyonzima alipokuwa akitambulishwa rasmi katika timu hiyo ya jangwani |
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Uganda na timu
ya Simba, Emmanuel Okwi, watachuana na kiungo wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya
Rwanda na Yanga Haruna Niyonzima kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka kwa
wachezaji wa kigeni nchini inayosimamiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (Taswa).
Mwingine wa kigeni alioingia kwenye
kinyang'anyiro hicho ni na Kipre Tchetche wa Ivory Coast anayechezea Azam FC.
Akizungumza katika hafla fupi ya kutaja
majina ya wachezaji wa ndani na nje watakaowania tuzo hizo, Mwenyekiti wa
kamati ya tuzo hizo Masoud Sanan alisema kwa upande wa wanasoka wazalendo,
wanaowania ni John Bocco, Aggrey Morris wote wa Azam na Juma Kaseja wa Simba.
Kwa kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje ya nchi ni Henry
Joseph wa Kongsvinger ya Norway
na Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC.
No comments:
Post a Comment